.RU

Title: The Holy Bible: Swahili New Testament - старонка 68


^14Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi

kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa?

^15Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula.

^16Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: "Nendeni salama mkaote moto na

kushiba," bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?

^17Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.

^18Lakini mtu anaweza kusema: "Wewe unayo imani, mimi ninayo matendo!"

Haya! Nionyeshe jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani bila matendo, nami

nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.

^19Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo

huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.

^20Mpumbavu wee! Je, wataka kuonyeshwa kwamba imani bila matendo

imekufa?

^21Je, Abrahamu baba yetu alipataje kukubalika mbele yake Mungu? Kwa

matendo yake, wakati alipomtoa mwanae Isaka sadaka juu ya madhabahu.

^22Waona basi, kwamba imani yake iliandamana na matendo yake; imani

yake ilikamilishwa kwa matendo yake.

^23Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: "Abrahamu

alimwamini Mungu na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na

hivyo Abrahamu akaitwa rafiki wa Mungu."

^24Mnaona basi, kwamba mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendo yake

na si kwa imani peke yake.

^25Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa

mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende

zao kwa kupitia njia nyingine.

^26Basi, kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila

matendo imekufa.

__________________________________________________________________

Chapter 3

^1Ndugu zangu, wengi wenu msiwe walimu. Kama mjuavyo, sisi walimu

tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine.

^2Lakini kama mtu hakosi katika usemi wake, basi, huyo ni mkamilifu, na

anaweza kutawala nafsi yake yote.

^3Sisi huwatia farasi lijamu kinywani mwao ili watutii; na kwa njia

hiyo twaweza kuwaongoza kokote tunakotaka.

^4Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali,

huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha

anakotaka.

^5Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia

makuu sana. ic Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.

^6Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo

nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote.

Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.

^7Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe

vyote--wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini.

^8Lakini hakuna mtu aliyeweza kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu,

hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.

^9Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huohuo

twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

^10Maneno ya laana na ya kusifia hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu

zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.

^11Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja?

^12Ndugu zangu, je, mti wa mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu

waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji

matamu.

^13Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aonyeshe

jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema

yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.

^14Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi,

msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.

^15Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya

ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.

^16Maana popote palipo na wivu na ubinafsi hapo pana fujo na kila aina

ya uovu.

^17Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani,

upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema;

haina ubaguzi wala unafiki.

^18Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika

amani.

__________________________________________________________________

Chapter 4

^1Mapigano na magombano yote kati yenu yanatoka wapi? Hutoka katika

tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu.

^2Mnatamani vitu na kwa vile hamvipati mko tayari kuua; mwatamani sana

kupata vitu, lakini hamvipati, hivyo mnagombana na kupigana. Hampati

kile mnachotaka kwa sababu hamkiombi kwa Mungu.

^3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili

mpate kutosheleza tamaa zenu.

^4Ninyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa

rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki

wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu.

^5Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure,

yanaposema: "Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu ana wivu mkubwa."

^6Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo

Maandiko: "Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema

wanyenyekevu."

^7Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni.

^8Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi

wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!

^9Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na

furaha yenu iwe huzuni kubwa.

^10Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni.

^11Ndugu, msilaumiane ninyi kwa ninyi. Anayemlaumu ndugu yake na

kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu Sheria. Kama ukiihukumu Sheria,

basi, wewe huitii Sheria, bali waihukumu.

^12Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka Sheria na kuhukumu. Ni yeye peke

yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu

binadamu mwenzako?

^13Basi, sasa sikilizeni ninyi mnaosema: "Leo au kesho tutakwenda

katika mji fulani na kukaa huko mwaka mzima tukifanya biashara na

kupata faida."

^14Ninyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kama

ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.

^15Mngalipaswa kusema: "Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki au

kile."

^16Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni

mabaya.

^17Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa

kulifanya, anatenda dhambi.

__________________________________________________________________

Chapter 5

^1Na sasa sikilizeni enyi matajiri! Lieni na kuomboleza kwa sababu ya

taabu zitakazowajieni.

^2Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo.

^3Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi

dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Ninyi mmejilundikia

mali katika siku hizi za mwisho!

^4Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu.

Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu

kimefika masikioni mwa Bwana, Mwenye Nguvu.

^5Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepesha

tayari kwa siku ya kuchinjwa.

^6Mmemhukumu na kumwua mtu asiye na hatia, naye hakuwapigeni.

^7Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni

mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno mazuri. Yeye

hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.

^8Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku

ya kuja kwake Bwana inakaribia.

^9Ndugu zangu, msinung`unikiane ninyi kwa ninyi msije mkahukumiwa na

Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia.

^10Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso,

fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana.

^11Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za

uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana

Bwana amejaa huruma na rehema.

^12Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia,

wala kwa kitu kingine chochote. Semeni "Ndiyo" kama maana yenu ni

ndiyo, na "La" kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu.

^13Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa kusali.

Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.

^14Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao

watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

^15Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na

dhambi alizotenda zitaondolewa.

^16Basi, ungamanianeni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa.

Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.

^17Eliya alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvua isinyeshe,

nayo haikunyesha nchini kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.

^18Kisha akaomba tena, mvua ikanyesha kutoka angani na nchi ikatoa

mazao yake.

^19Ndugu zangu, mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, na mwingine

akamrudisha,

^20fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia yake

ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi

zitaondolewa.

__________________________________________________________________

1 Peter

__________________________________________________________________

Chapter 1

^1Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo nawaandikia ninyi wateule wa Mungu

Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia,

Kapadokia, Asia na Bithunia.

^2Mungu Baba aliwateua ninyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa

watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu

yake. Nawatakieni neema na amani tele.

^3Asifiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa huruma yake kuu

alitufanya tuzaliwe upya kwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Ametujalia

tumaini lenye uzima,

^4na hivyo tunatazamia kupata baraka zile ambazo Mungu aliwawekea watu

wake. Mungu amewawekeeni baraka hizo mbinguni ambako haziwezi kuoza au

kuharibika au kufifia.

^5Hizo zitakuwa zenu ninyi ambao kwa imani mnalindwa salama kwa nguvu

ya Mungu kwa ajili ya wokovu ambao uko tayari kufunuliwa mwishoni mwa

nyakati.

^6Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo,

itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka.

^7Shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe ambayo

huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu ambayo ni

ya thamani zaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa

thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima Siku ile Yesu Kristo

atakapofunuliwa.

^8Ninyi mnampenda ingawaje hamjamwona, na mnamwamini ingawa hamumwoni

sasa. Hivyo, mnafurahi kwa furaha tukufu isiyoelezeka,

^9kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu.

^10Manabii walipeleleza kwa makini na kufanya uchunguzi juu ya wokovu

huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo ninyi mngepewa.

^11Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati

alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya

mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.

^12Mungu aliwafunulia kwamba wakati walipokuwa wanasema juu ya hayo

mambo ambayo ninyi mmekwisha sikia sasa kutoka kwa wale wajumbe

waliowatangazieni Habari Njema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyetumwa

kutoka mbinguni, hiyo kazi yao haikuwa kwa faida yao wenyewe, bali kwa

ajili yenu. Hayo ndiyo mambo ambayo hata malaika wangependa kuyafahamu.

^13Kwa hiyo, basi, muwe tayari kabisa kwa nia, na kukesha. Wekeni

tumaini lenu lote katika baraka ile mtakayopewa wakati Yesu Kristo

atakapoonekana!

^14Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tamaa

mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga.

^15Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile

yule aliyewaiteni ni mtakatifu.

^16Maandiko yasema: "Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu."

^17Mnapomtaja Mungu ninyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye

humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo

tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.

^18Maana mnajua kwamba ninyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa

ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu, si kwa vitu vyenye kuharibika:

kwa fedha na dhahabu;

^19bali mlikombolewa kwa damu tukufu ya Kristo, ambaye alikuwa kama

mwana kondoo asiye na dosari wala doa.

^20Yeye alikuwa ameteuliwa na Mungu kabla ya ulimwengu kuumbwa,

akafunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu.

^21Kwa njia yake, ninyi mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka wafu na

kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.

^22Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, ninyi mmezitakasa roho zenu na

kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.

^23Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, ninyi mmezaliwa upya, si kama

watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.

^24Kama Maandiko yasemavyo: "Kila binadamu ni kama nyasi, na utukufu

wake wote ni kama maua ya porini. Nyasi hunyauka na maua huanguka.

^25Lakini neno la Bwana hudumu milele." Neno hilo ni hiyo Habari Njema

iliyohubiriwa kwenu.

__________________________________________________________________

Chapter 2

^1Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa

visiweko tena.

^2Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa

kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua

na kukombolewa.

^3Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mmegundua kwamba Bwana ni

mwema."

^4Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu;

lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule, na la thamani kubwa.

^5Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho,

ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea dhabihu za kiroho
2010-07-19 18:44 Читать похожую статью
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • Контрольная работа
 • © Помощь студентам
  Образовательные документы для студентов.